Kocha
wa Arsenal Arsene Wenger amepewa ruhusa ya kumnunua mshambuliaji wa
Manchester United Wayne Rooney endapo atahisi kuwa mchezaji huyo
anahitajika kwenye klabu yake .
Mkurugenzi mtendaji wa Arsenal Ivan Gazidis amesema kuwa klabu yake ina uwezo wa kumnunua Wayne Rooney kwa paundi milioni 25 pamoja na mshahara wa paundi 200,000 kwa wiki sawa na anaolipwa kwenye klabu ya Manchester United kwa sasa .
Akizungumza na gazeti la The Sun la nchini England , Gazidis ameongeza kuwa kama Arsene Wenger akipeleka maombi a kumnunua mchezaji yo kwenye bodi ya wakurugenzi hakuna atakayekataa kwa kuwa iko kwenye uwezo wao kama labu kufanya manunuzi hayo pamoja na kumudu kumlipa mshahara.
Wayne Rooney amekuwa kwenye wakati mgumu siku za hivi karibuni huku akitafakari mustakabali wake wa baadae ndani a United baada ya kuomba kuuzwa mwishoni mwa msimu ulipita . Hata hivyo ripoti nyingine zimezema kuwa Rooney anajiandaa kufanya uamuzi w kubaki ndani ya United baadaya kustaafu kwa Sir Alex Fergusson mtu ambaye hawakuwa na uhusiano mzuri siku za hivi karibuni.
Klabu kadhaa zimekuwa zikifuatilia maendeleo ya Wayne Rooney ndani ya Old Trafford zikijiandaa kumnunua endapo mchezaji huyo atafikia maamuzi ya kuondoka United ,baadhi ya klabu hizo ni Arsenal na Paris St Germain ambao wameenda mbali zaidi na kudai kuwa wako tayari kumlipa Rooney paundi 300,000 kwa wiki endapo atasaini kwenye klabu hiyo.

0 comments:
Post a Comment